MICHAEL MTANZANIA

ONESTEPMEDIATZ

IFAHAMU HUKUMU ILIYOTOLEWA NA ALIYEKUWA RAISI WA IRAQ SADDAM HUSSEIN ILIYOPELEKEA MADAKTARI KUKATWA MIKONO

 
Kuanzia Juni 4, 1994 serikali ya Iraq chini ya Saddam Hussein ilitoa amri tisa ambazo zikikiukwa tuu adhabu yake ilikuwa ni kali kama vile kukatwa viungo vya mwili, kupigwa chapa au adhabu ya

kifo, baadhi ya makosa yaliyopelekea adhabu hizo ni kama vile wizi, ufisadi au rushwa.


Amri hizi mpya ziliathiri sana haki za binadamu lakini serikali ya Iraq ilipuuza ukosoaji mkubwa wa kimataifa wa ukatili huu kwa kusema kwamba amri hizo zilitungwa ili kupambana na uhalifu nchini humo ambapo unaleta vikwazo vya kiuchumi.

Miaka hiyo ya 1990 afisa mmoja wa nchini humo alituhumiwa kwa rushwa na wizi wa fedha za serikali, alikatwa mikono yake pamoja na kupigwa chapa isiyofutika katika maeneo ya uso.

Jamaa akaamua kwenda hospitali akafanyiwe plastic surgery ili chapa hiyo ifutike, ni kweli alifanikiwa lakini alivyobainika tuu madaktari waliobainika kumfanyia upasuaji huo pia walikamatwa, walikatwa mikono na Kupigwa chapa ya alama hiyo hiyo pia.

Mwaka huo huo 1994 zaidi ya watu 300 walikutwa katika kambi moja ya jeshi mjini Kurdistan wakiwa wamekatwa masikio, walionekana wamepigwa chapa ya X pia isiyofutika katika eneo la uso.

Anaitwa Saddam Hussein aliyezaliwa April 28, 1937 na kufariki Dec 30, 2006 kwa kunyongwa huko Kadhimiya, Baghdad, Iraq akiwa na miaka 69. Aliwahi kuwa rais wa awamu ya 5 wa Iraq 1979-2003, aliwahi pia kuwa makamu wa rais wa Iraq 1968-1979.

Saddam alihukumiwa kifo kwa kunyongwa huko Iraq baada ya kupatikana na hatia ya mauwaji ya makusudi dhidi ya watu, ambapo aliwauwa viongozi wakubwa 148 wa kishia huko Dujail mwaka 1982 ili kulipiza kisasi kwa jaribio la mauaji walilowahi kulifanya dhidi yake. Dujail ni mji wenye waislam wengi wa Kishia huko Iraq.

Wakati Saadam anatimiza umri wa miaka 60 mwaka 1997 alitangaza kuwa aliamua kukikopi kitabu kitukufu cha Kiislam cha Kuruani na kukiandika chakwake kwa kutumia damu yake kama wino aliyokuwa akiitoa mwilini mwake kwa zaidi ya miaka miwili. Iliita Blood Qur'an.

Alisema kuwa alikuwa amekiandika kitabu hicho kwa kutumia lita 27 za damu yake, kila akijitoa damu inatumika kuandika, kwahivyo hadi miaka hiyo miwili inakatika alikuwa ametoa lita 27. Kiafya lita 27 za damu zilipaswa kumchukua hadi miaka 9 kuzitoa.

Miaka mitatu baadae Septemba 2000 aliandika barua na kuiweka wazi kupitia vyombo vya habari akisema kuwa lengo la kuandika kitabu hicho ilikuwa ni kutoa sadaka kwa Mungu, kumshukuru Mungu kwa kumsaidia kuokoka katika majaribio mengi ya hatari ya kuwawa dhidi yake.

"Maisha yangu yamejaa hatari ambayo ningepoteza damu nyingi sana, lakini kwa kuwa nimepoteza damu kidogo, nimeona niandike maneno ya Mungu kwa damu yangu mwenyewe kama shukrani." Alizungumza Saadam Hussein mwaka 1997.

Mwaka 2000 kitabu hicho kilipokelewa na viongozi wakubwa wa kidini wa Falme za Kiarabu na Saudi Arabia, na baada ya Saddam kutolewa madarakani mwaka 2003 Kuruani hiyo imefungiwa katika sehemu ya siri sana huko Baghdad huku viongozi wakiwa hawajui waitumie vipi.

Inaelezwa kuwa Makasisi wa Kiisilamu wamebaki njiapanda juu ya uamuzi wa ama kukiharibu kitabu hicho au kukihifadhi kama ukumbusho wa kiongozi huyo, hofu hiyo inakuja baada ya kuamini kuwa Saddam hakuitendea haki Qur'an.

Saddam Hussein

Saddam Hussein

Saddam Hussein



Post a Comment

0 Comments