Horacio Corbacho & Nicola Corradi |
Mwaka jana 2019 nchini Argentina kulikuwa na taarifa kubwa iliyowagusa wengi ikiwahusu watawa wa kanisa katoliki mjini Mendoza waliohukumiwa zaidi ya miaka 40 jela kila mmoja kufuatia tuhuma za
kuwaingilia kingono wanafunzi wakike walemavu wa masikio katika shule moja ya kanisa nchini humo.Mtawa Horacio Corbacho alihukumiwa kifungo cha miaka 45 jela wakati mtawa mwenzake Nicola Corradi raia wa Italia alihukumiwa miaka 42 jela huku watawa wengine zaidi ya wanne wakihukumiwa pia.
Wote walishtakiwa kwa kuwaingilia kingono zaidi ya wasichana 20 walemavu wa masikio waliokuwa wakilelewa katika kituo cha kulelewa watoto wa kike viziwi ya Provolo Institute for deaf and hearing-impaired ya nchini humo, makosa waliyoyafanya kati ya mwaka 2004-2016.
Hawa 20 ndio waliothibitika moja kwa moja kufanyiwa vitendo hivyo, iliaminika kuwa kulikuwa na idadi zaidi ya hiyo.
Uchunguzi ulianza kufanyika baada ya wafanyakazi wa kufua nguo za watoto hao walipoona hali ya uwepo wa damu katika nguo za ndani wakati wanafua imezidi kwa miezi mingi, wakaamua kuripoti polisi.
Wafanyakazi hao walisema kuwa hakuna yeyote aliyekuwa anasikia watoto hao wakipiga kelele wakifanyiwa vitendo hivyo miaka ypte kutokana na wote kuwa walemavu wa masikio.
Ajabu zaidi ni kwamba wafanyakazi wengi kituoni hapo walikuwa ni watawa wakike, hawa ndio walikuwa wanawasaidia watawa wakiume waliokuwa wanasafiri kutoka mbali kuja kuwapata kingono watoto hao.
Pichani ni mtawa wa kike Kosaka Kumiko (42) akiwa chini ya ulinzi mkali wa Polisi.
0 Comments