MICHAEL MTANZANIA

ONESTEPMEDIATZ

Nape atema cheche kwa maofisa habari

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amemwagiza Mkurugenzi wa Habari Maelezo kufuatilia utendaji kazi wa maofisa habari na mawasiliano wote ili kujiridhisha kama wanafanya kazi zao kwa mujibu wa sheria.
Waziri huyo ametoa kauli hiyo Jumanne hii wakati akizungumza na maofisa habari na mawasiliano wakati akifungua kikao kazi cha 12 cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali kinachofanyika mkoani Dodoma.
“Nataka niiagize ofisi ya Mkurugenzi wa habari maelezo kuhakikisha kuwa mnafuatilia utendaji kazi wa kila ofisa habari na mawasiliano ili kujiridhisha kama wanafanya kazi zao kwa mujibu wa sheria au la na kama tutabaini kuna ofisa habari ambaye hatekelezi majukumu yake ipasavyo tumwombe atupishe.”
Ameongeza “Kutoa habari zinazohusiana na taasisi zenu mnazofanyia kazi ni jukumu lenu la kisheria na siyo hiari yenu kwa hiyo hakikisheni kuwa waandishi wa habari wanapowatafuta ili kupata habari kwenye ofisi zenu mnawapa taarifa sahihi na kwa wakati ili jamii iweze kupata majibu ya maswali yao kwa wakati na kwa usahihi.”

Post a Comment

0 Comments