Benki
ya NBC imemshitaki Mfanyabiashara na aliyekuwa Mwwenyekiti wa klabu ya
Yanga, Yusuf Manji kwa kushindwa kulipa mkopo wa shilingi bilioni 26.
Taarifa kwa mujibu wa gazeti la Dailu News limeeleza kuwa Manji amekuwa miongoni mwa wafanyabiashara hao wakiwemo wengine wanne wanaodaiwa kiasi hicho cha fedha.
Daily News liemandika kuwa NBC wamemfungulia Manji mashitaka na wenzake katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Biashara ambapo madai ya kwanza ni juu ya Farm Equip (Tanzania) Company Limited, na Manji na watu wengine wanaosimama kama wadhamini.
Wadaiwa wengine katika mkopo huo ni pamoja na Tanperch Limited, Quality Group Limited na Kaniz Manji. Mkopo wa pili ulikwenda kwa Tanperch Limited, ikiripotiwa umedhaminiwa na Manji, Quality Group Limited na Kaniz Manji, ambao pia ni wahusika.
Daily News wamednaika wakieleza kwa mujibu wa brua iliyochapishwa kwenye vyombo vya habari hivi karibuni, imeeleza washitakiwa hao wanatakiwa kuwasili mahakamani wao wenyewe au watume mawakili wao Juni 25 2018 kesi hiyo itakaposikilizwa.
Wakati wakuchukua mikopo hiyo, mali zisizohamishika pamoja na mejengo ziliwekwa kama dhamana ikiwa na pamoja na viwanja vitatu vilivyopo jijini Mwanza, Ilemela.
Jengo la Quality Group Limited ni miongoni mwa mali zilizowekwa kama dhamana na endapo mkopo hautarudi litawezwa kupigwa mnada ili kufikidia madeni ya madeni ya Farm Equip (Tanzania) Company Limited.
0 Comments