MICHAEL MTANZANIA

ONESTEPMEDIATZ

DITRAM NCHIMBI ATAMBULISHWA RASMI AZAM


Rasmi uongozi wa Azam FC umemtambulisha aliyekuwa Mshambuliaji wa Njombe Mji, Ditram Nchimbi, baada ya kuingia naye mkataba wa miaka miwili.

Nchimbi amejiunga Azam akitokea Njombe Mji iliyoteremka daraja katika msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara.

Ujio wa Nchimbi ndani ya kikosi cha Azam umezidi kuongeza wachezaji wapya watakaokuwa na timu hiyo msimu ujao baada ya usajili wa Donald Ngoma na Tafadzwa Kutinyu.

Mchezaji huyo ataungana na wenzake hivi karibuni tayari kuanza mazoezi kwa ajili ya mashindano ya Kagame yanayotarajia kuanza Juni 28 mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments