MICHAEL MTANZANIA

ONESTEPMEDIATZ

Serikali kuchunguza mali za viongozi zaidi ya 900, yaeleza sababu za uchunguzi huo

    Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela amesema kuwa wamefanya uchambuzi ambapo kwasasa zaidi ya viongozi 900 wanahakikiwa mali zao.
    Akizungumza na Wanahabari leo, Juni 11, 2018, Nsekela amesema kuwa sababu ya kwanza iliyofanya kuhakiki mali hizo ni kudhibitisha tamko walilopeleka na uhalisia wa mali hizo.
“Sasa tumefikia mahali ambapo tuende kuhakiki kwa baadhi ya viongozi nasema kwa baadhi ya viongozi kwasababu kuna sababu nyingi, sababu kubwa tunasema ni rasilimali fedha tunasema kwamba kama fedha hatuna za kutosha hatuwezi kuwahakiki viongozi wengi kwa hivi sasa tumefanya uchambuzi wa viongozi 900 ambao sasa tunakwenda kuwahakiki mnaweza mkasema mnahakiki kwa sababu gani, sababu ya kwanza ni kudhibitisha uhalisia wa mali hizo kulinganisha na tamko walilotuletea, tunatafuta thamani ya hizo mali walizonazo hao viongozi na uhalali wa hizo mali kwa maana ya kwamba hizo mali walizipataje” amesema Nsekela.
Nsekela ameongeza “Kama mnavyojua sisi tunazungumzia suala zima la Maadili kwamba kiongozi awe na Maadili na mimi kama kiongozi na mmoja wapo wa viongozi nikitoa tamko langu na nikitaka kuhakiki tunataka tujue zile mali nilizo nazo na uwezo wangu kuna uwiano gani hapo, hizo mali nimepata kihalali au sijapata kihalali, kwahiyo unaweza ukauliza maswali mengi hapo,kwahiyo sababu kubwa la kwenda kuhakiki hizo mali ni hiyo hapo, kuangalia uhalali wa mali za sisi viongozi jinsi zilivyopatikana, maana yake ni kwamba sisi viongozi tunatakiwa tuwe na mali zilizopatikana kihalali na sio vinginevyo kwahiyo ndiyo zoezi kubwa tunaloenda kulifanya kuanzia tarehe 18 mwezi huu ndio tutaanza zoezi hilo la kuhakiki hao viongozi tuliowachagua na litatuchukua wiki nne au mwezi mmoja nadhani mpaka tarehe 18 mwezi July na kwasababu ni zoezi nyeti, tumeona ni vizuri viongozi kwanza tuwaambie kwamba kuna zoezi hilo linakuja.”
Ikumbukwe Disemba 27, 2017 Nsekela aliwahimiza Viongozi wa Umma kukamilisha taratibu za ujazaji wa fomu za tamko la rasilimali na madeni kabla ya Disemba 31 mwaka huo.

Post a Comment

0 Comments