Lechantre alishukuru wakati benchi la ufundi likipewa tuzo maalum ya shukurani, naye aliwaongoza wasaidizi wake, Masoud Djuma na Mohammed Habib.
Baada ya kushukuru kwa tuzo hiyo, Lechantre alisema anawatakia Simba kila la kheri katika muendelezo mzuri wa mambo.
Ingawa hakusema moja kwa moja ilionyesha wazi kocha huyo amekamilisha ile ishu yake, kwamba anaondoka Simba.
Tayari uongozi wa Simba umeanza mchakato wa kusaka kocha na Selemani Matola kutoka Lipuli ni kati ya wanaopewa nafasi ya kuongeza nguvu.
Hata hivyo, kuna taarifa Simba imekuwa ikisaka kocha nje ya bara la Afrika kuchukua nafasi ya Mfaransa huyo ambaye huenda akaondoka kesho au keshokutwa kurejea kwao.
0 Comments