Kuelekea mechi ya Simba SC dhidi ya Kagera Sugar, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara, amesema atajitolea kuwalipia mashabiki kiingilio.
Manara amefikia uamuzi kutokana na hitaji lake la kuwataka wanachama na wapenzi wa Simba kujitokeza kwa wingi katika mechi hiyo ambayo itahudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.
Akizungumza na Radio EFM kupitia Sports HQ, Manara ameeleza kuwa kwa wale baadhi watakaokuwa hawana fedha za kiingilio, atakuwepo getini na bunda le fedha kuwapatia Tshs 2000 kwa kila mmoja.
Mbali na kujitolea kiingilio, Manara amewaomba watani zake wa jadi Yanga kuja kwa wingi Uwanjani hata kama watakuja kuzomea huku akieleza kuwa hiyo ndiyo burudani ya soka.
Mechi hiyo dhidi ya Kagera itaenda sambamba na Simba kukabidhiwa kombe la ligi waliloshinda msimu huu ambapo Rais Magufuli ndiye atakayewakabidhi taji hilo.
0 Comments