Kocha Zahera Mwinyi baada ya kuwasili kwa lengo la kuifundisha klabu ya
Yanga ilionekana alikuwa bado hajasaini mkataba, hatimaye kocha huyo
amesaini mkataba wa kuifundisha klabu hiyo.
Hussein Nyika mwenyekiti wa kamati ya usajili Yanga amethibisha kocha huyo kusaini mkataba wa miaka miwili.
“Tumemalizana na mwalimu siku ya Ijumaa amesaini mkataba kwa ajili ya
kuifundisha Yanga lakini kesho (Jumamosi) anataraji kuondoka kwenda DR
Congo kwa ajili ya majukumu ya timu ya taifa kwa sababu mwalimu huyo
tulimchukua wakati yupo kwenye majukumu ya kitaifa.”
“Kwa hiyo anakwenda kutimiza majukumu yake kwa sababu timu ya DR Congo
ina mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Nigeria weekend ijayo.”
“Atarejea Tanzania baada ya wiki moja kutoka kwenye mechi ya kirafiki kati ya DR Congo dhidi ya Nigeria.”
Nyika amefafanua kwa nini Zahera alikuwa haikai kwenye benchi la ufundi
la Yanga katila mechi zilizochezwa tangu alipowasili Yanga.
“Nafikiri watu walikuwa hawaelewi kwa sababu gani mwalimu alikuwa
anashindwa kukaa kwenye benchi, ni kwa sababu hakuwa na mkataba, huwezi
kupata kibali cha kufanya kazi kama hauna mkataba wa kufanya kazi sehemu
ambayo unatakiwa kufanya kazi.”
“Baada ya kusaini mkataba, kuanzia Jumatatu tunashughulikia vibali vyake
kwa ajili ya kuitumikia Yanga. Kwa hiyo mpaka atakapo rudi atavikuta
vibali vitakuwa tayari na ataanza kukaa kwenye benchi la Yanga.”
0 Comments