Kocha Mtarajiwa wa Yanga, Mkongomani Mwinyi Zahera, ameondoka nchini kuelekea kwao Congo kwa ajili ya majukumu ya timu ya taifa.
Zahera ambaye ni Kocha Msaidizi wa Congo ameondoka huku Yanga ikiwa inajiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Mwadui FC utakaopigwa kesho kwenye Uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga.
Kocha huyo bado hajasaini mkataba wa kuitumikia Yanga mpaka sasa na taarifa zinaelezwa kuwa bado wapo kwenye mazungumzo ya kumalizana naye taratibu.
Shadrack Nsajigwa pamoja na Noel Mwandila ndiyo wamekabidhiwa majukumu ya kuinoa Yanga ambayo vilevile inashiriki mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Haijaelezwa Zahera atarejea lini lakini ameondoka nchini huku akiwa amewaaga viongozi wa Yanga ili kupata nafasi ya kwenda kutimiza majukumu ya Congo ambayo inajiandaa na mechi za Kombe la Mataifa ya Afrika.
0 Comments