Taarifa zinaelezaa kuwa Kocha Mkuu wa Singida United, Kocha Hans van der Plujim ameuaga uongozi wa klabu yake ya Singida kwa madai ya kuwa anaondoka.
Pluijm alijiunga na kikosi cha Singida mapema mara baada ya timu hiyo kupanda daraja msimu uliopita wa 2016/17 akitokea katika klabu ya Yanga.
Hivi karibuni kumekuwa na taarifa zinazosema kuwa Kocha huyo atatuta Azam FC kuchukua mikoba ya Mromania Aristica Cioba aliyeondoshwa baada ya kushindwa kufanya vizuri na timu hiyo msimu huu.
Yawezekana ikawa ni safari rasmi ya kuelekea Azam FC ambayo imetajwa kumsajii tayari kuchukua nafasi ya Mromania aliyeondoka na tayari kukiongoza katika maandalizi ya msimu ujao.
0 Comments