Zifutazo ndizo hatua tano jinsi ya kuwa mfanyabiashara mwenye mafanikio.
1. Ainisha aina za biashara ambazo unataka kuzifanaya.
Katika hili ni kwamba kama unataka kuwa mfanyabiashara mwenye mafanikio, unatakiwa kuanisha aina mbalimbali za biashara ambazo unataka kuzifanya,huenda zikawa ni zaidi ya biashara hata sita. Ukishapata biashara hizo jaribu kuwashirikisha hata baadhi ya ndugu na jamaa ili wakupe mtazamo wao ni biashara ipi amabayo inafaa.
2.Chagua biashara moja ambayo unaiona inafaa.
Hatua ya pili baada ya kuwashirikisha ndugu na jamaa, unachotakiwa kufanya ni kwamba kaa chini pamoja na halmashauri yako ya kichwa ili kuweza kupambanua ni biashara ipi amabayo inafaa, baada ya kupata majibu tafakari kisha chagua mwenyewe biashara moja amabayo itakuwa na faida kwako hapo mbeleni.
Angalizo; kuwa makini katika kuchagua wazo la biashara kwani kukosea kuchagua wazo bora la biashara ni sawa na kukosea kuoa mke.
3. Fanya utafiti juu ya washidani wako.
Baada ya kupata wazo moja la biashara hatua ya tatu ni kwamba unatakiwa kufanya utafiti wa juu ya washindani wako ambao tayari umewakuta wakifanya biashara. Na katika kufanya utafiti wako unatakiwa kujua ni mbinu zipi ambazo wao huzitumia katika kuapata wateja, baada ya kujua hii itakusaidia ili kujua mbinu mpya ambayo itakufanya uweze kuwavuta baadhi ya wateja ili waje kwako.
Lakini nikuibie siri moja hakuna siri kubwa katika mafanikio makubwa ya kibiashara kama kuwa mbunifu, ubunifu ndio siri na siraha makini ya utendaji wako wa kibiashara yenye mafanikio.
4. Tengeneza mpango wa biashara hiyo.
Baada ya kujua mbinu za kuwatambua na kuwashida washindani wako, jambo la nne ni kuhakikisha unandaa mpango biashara amabao ndio utakao ongoza biashara yako. Katika mpango wa biashara ndio ambao utakusaidia kwa kiwango kikubwa kujua biashara yako jinsi ambavyo utakavyokuwa. Nakusihi tu uendelee kufuatana nami afisa mipango kila wakati nitakueleza siku nyingine jinsi ya kuandaa mpango wa biashara.
5. Tafuta mtu atakayekuongoza na kukusimia katika biashara hiyo.
Mwisho kabisa ili uweze kufanikiwa katika biashara unahitaji kuwa na mtu wa kukuongoza katika biashara yako. Mtu huyu anatakiwa kuwa mzoefu katika biashara ambayo unaifanya, uzoefu wa mtu huyo litakuwa darasa tosha kwako kwa kukuelekeza ni nini ufanye na nini usifanye.
Asante kwa kuwa nami katika makala haya ni wajibu wangu kuhakikisha unaimarika kifikra kila wakati.
0 Comments