Kwa sasa umekuwa ni mtindo wa kawaida watu kuwafungulia watoto
wao akauti Instagram ili kuwawekea picha zao. Leo ningependa kukuletea
top ten ya watoto wa wastaa ambao wapo Instagram, orodha imepangwa kwa
kuzingatia idadi ya followers.
1. Tiffah wa Diamond & Zari
Katika akaunti yake watu zaidi ya milioni 1.2 wanamfuata, huku yeye akiwafuata watu watatu tu ambao ni pamoja na wazazi wake, huku
akituma picha 819.
2. Cookie wa Aunty Ezekiel & Mose Iyobo
Huyu watu zaidi ya 274,000 wanamfuatilia katika akauti yake, huku yeye akiwafuata watu watu wawili tu ambao ni wazazi wake, ameshatuma picha 206.
3. Nillan wa Diamond & Zari
Watu takribani 200,000 wanamfuatilia, huku yeye akiwafuata watu watatu ambao ni wazazi wake na dada yake (Tiffah) na ameshatuma picha 81.
4. Mali wa Ben Pol
Akaunti yake yenye jina Maliboard ina followers 124k, amefuata watu 99 na kuweka picha 27.
5. Tanzanite wa H Baba & Flora Mvungi
Malkia huyu anafuatwa na watu zaidi ya 77,000 huku yeye akiwafuata watu 62 na ametuma picha 3142.
6. Mozzah wa Aslay
Huyu watu zaidi ya 73,000 wanamfuatilia huku yeye akiwafuata watu wawili tu akiwemo baba yake, hadi sasa ameshatuma picha 93.
7. Amaya wa Alikiba
Watu zaidi ya 35,000 wanamfuatilia, huku yeye akiwafata watu 22, na kutuma picha 129.
8. Kendrick wa Mabeste
Mtoto huyu wa rapa Mabeste anafuatwa na watu zaidi ya 33,000 huku yeye akimfuata mtu mmoja tu ambaye ni mdogo wake (Kaytly), ameshatuma picha 168.
9. Sasha wa Faiza Ally & Mr II ‘Sugu’
Katika akauti yake watu zaidi ya 30,000 wanamfuatilia, yeye hajamfuata mtu hata mmoja na hadi sasa ameshatuma picha 1189.
10. Jaden wa Ray Kigosi & Chuchu Hans
Huyu watu zaidi ya 27,000 wanamfuatilia, huku yeye akiwafuata watu wawili tu ambao ni wazazi wake, na ametuma picha 41.
11. Krish wa Irene Uwoya (Bonus)
Watu takribani 15, 000 wanaomfuta, wakati yeye akiwafuata watu 40 na kutuma picha 27.
0 Comments