MICHAEL MTANZANIA

ONESTEPMEDIATZ

Anachoamini Mkude baada ya Simba kufungwa 2-1 na Kagera Sugar


Baada ya Simba kupoteza mchezo wao wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Kagera Sugar kwa kuchapwa 2-1, nahodha wa Simba Jonas Mkude amesema bado wanaendelea kufukuzia ubingwa hadi mwisho kwa sababu bado ipo nafasi ya kushinda taji hilo ikiwa watafanya vizuri kwenye
mechi zao zilizosalia kwenye ratiba ya ligi.

“Ndiyo matokeo ya mchezo, tumepoteza mechi lakini bado hatukati tama, tutapambana hadi mwisho kuhakikisha tunashinda ubingwa wa ligi,” alisema Mkude mara baada ya mchezo wakati akizungumza na Azam TV.

“Nafasi bado ipo, sasa tunajipanga kwa ajili ya mechi zetu mbili zilizobaki huku Kanda ya Ziwa. Mashabiki waendelee kutuunga mkono wasife moyo bado tupo kwenye nafasi nzuri.”
Simba ina mechi mbili dhidi ya timu za mkoa wa mwanza (Toto Afrikans na Mabao FC)ambazo zote zinapambana kukwepa mkasi wa kushuka daraja hivyo Wekundu wa Msimbazi watakutana na upinzani mkali kutoka kwa timu hizo huku Toto Africans ikiwa na historia nzuri kuifunga Simba kwenye mechi za ligi.

Post a Comment

0 Comments