Kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi, Danny Blind hatimaye ametimuliwa kufuatia muendelezo wa matokeo mabaya kunako timu hiyo.
Maamuzi hayo yamekuja baada ya kipigo cha 2-0 kutoka kwa Bulgaria juzi jumamosi ambacho kimewafanya Uholanzi kushika namba 4 katika kundi lake la kufuzu michuano ya kombe la Dunia 2018 Russia.
Blind,55, ambaye alichukua nafasi ya kuifundisha timu hiyo kutoka kwa Guus Hiddink mwaka 2015, lakini akashindwa kuipeleka kwenye michuano ya
Euro Ufaransa mwaka jana.
Mholanzi huyo amepoteza mechi 5 kati ya 9 za ushindani ambazo ameiongoza Uholanzi tangu apewe kibarua hicho mwaka 2015.
Kipa wa zamani wa Ajax Fred Grim ndiye aliyeteuliwa kuwa kocha wa muda wa timu hiyo na ataiongoza kesho jumanne kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Italia.
0 Comments