Mr T Touch amethibitisha kumsajili Young Dee kwenye lebo yake, Touchez Sound Records kwa miaka mitatu.
Mtayarishaji huyo wa muziki amekiambia kipindi cha E-News cha EATV Ijumaa hii kuwa yeye atakuwa anasimamia kutengeneza beat za nyimbo zote za msanii huyo.
“Mimi nimeingia mkataba mrefu wa miaka mitatu na Young Dee. Ataendelea kuwepo chini ya
Touchez Sound na mimi ndiye nitakayesimamia na kutengeneza beat za nyimbo zake zote. Nia yangu ni kumfanya afanye vitu tofauti na alivyokuwa akifanya hapo awali kwa kuwa mimi namuona ni msanii mwenye biashara,” amesema Touch.
Young Dee alikuwa anasimamiwa kazi zake na MDB ya Max Rioba kabla ya kutangaza kuachana naye mapema mwanzoni mwa mwaka huu.
0 Comments