Baada
ya tetesi zilizojitokeza hivi karibuni kuwa uongozi wa Yanga upo
katika mipango ya kuwachukua wachezaji wa Simba, kiungo Jonas Mkude na
mshambuliaji Ibrahimu Ajibu, mabosi wa wachezaji hao wameibuka na
kusema kuwa ni ruksa kwa kuwa wachezaji hao wapo huru kufanya chochote
kutokana na mikataba yao kukaribia kufikia tamati.
Kuna
taarifa kuwa tayari kuna mipango imeanza
kufanywa ndani ya Yanga kuhakikisha wanawapata wachezaji hao kutokana na majina yao kutajwa kuwepo katika mchakato wa kusajiliwa msimu ujao wa ligi kuu kufuatia mikataba yao kumalizika huku Ajibu akitajwa kuwa katika rada zao kwa muda mrefu.
kufanywa ndani ya Yanga kuhakikisha wanawapata wachezaji hao kutokana na majina yao kutajwa kuwepo katika mchakato wa kusajiliwa msimu ujao wa ligi kuu kufuatia mikataba yao kumalizika huku Ajibu akitajwa kuwa katika rada zao kwa muda mrefu.
Aidha,
Mkude na Ajibu ni miongoni mwa wachezaji wanaotarajia kumaliza mikataba
ndani ya Simba mwezi wa sita mara baada ya ligi kufikia tamati ambapo
hadi sasa wamegoma kufanya mazungumzo ya kuongeza mkataba mwingine wa
kuitumikia timu hiyo kwa madai kuwa wanasubiria hadi watakapomaliza
rasmi mikataba yao mwishoni mwa ligi ndipo wafanye maamuzi.
Akizungumza na Championi Jumatatu,
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe alisema
kuwa, iwapo kuna watu wanafanya mazungumzo na wachezaji wao hao
waendelee kwa kuwa hawawezi kuwazuia kwa kuwa ni wachezaji huru ambao
mikataba yao inakaribia kumalizika.
“Kama
kuna watu wanafanya nao mazungumzo waache tu waendelee kuzungumza nao,
mimi sijui chochote, watu wamekuwa wakiniuliza sana kuhusiana na jambo
hilo, kwa upande wetu muda bado wa kuweza kuzungumzia suala hilo, ila
tunachojua bado ni wachezaji wetu na hawajamaliza mikataba yao hadi
mwisho wa ligi.
“Kwa
sasa Ajibu na Mkude ni wachezaji huru popote wanaweza kwenda kama Yanga
wamefanya nao mazungumzo ni sawa, kwani mchezaji akiwa anakaribia
kumaliza mkataba anakuwa huru hivyo ni ruksa kuzungumza na timu
nyingine, kusema watu wa Yanga wanawahitaji mimi hainihusu na wala
siwezi kuwazuia, ni ruksa kwenda kokote.
“Kwa
sasa mtazamo wetu wote ni kwenye ligi na tutakapofikia huko tutasema
kinachoendelea, wakati wa usajili bado,” alisema Hanspope.
0 Comments