WAKATI Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli akimpongeza msanii wa muziki, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwa kujaaliwa kupata mtoto wa pili ambaye ni Nillan, baba mzazi wa msanii huyo, Juma Abdul amesema kuna ulazima wa mjukuu wake huyo kupima DNA ili kuzima zile tetesi kuwa, si wake.
Rais Magufuli alimpongeza Diamond Jumanne wiki hii baada ya kiongozi huyo wa nchi kupiga simu kwenye Kipindi cha 360 cha Clouds TV wakati Diamond akihojiwa ambapo alisema: “Hongera sana Diamond kwa kumpata mtoto mwingine, wakati wa kampeni ulikuwa na mtoto mmoja, sasa umeongeza wa pili, nakupongeza sana.”
ISHU YA DNA SASA…
Awali, baada ya Zarinah Hassan ‘Zari’ kujifungua mtoto huyo nchini Afrika Kusini, yaliibuka madai mtandaoni kuwa, mtoto huyo anafanana sana na aliyekuwa mume wa Zari, Ivan Semwanga na kwamba kuna uwezekano uchepukaji ulichukua nafasi yake. Madai hayo yaliyofanana na yale ya kipindi kile Diamond alipompata Tiffah, yalishika kasi na kufikia wakati baadhi wakawa wanaunganisha picha ya Nillan na Ivan kisha kuonesha jinsi sehemu nyingi za usoni zilivyofanana.
Licha ya maneno hayo kuenea kila kona na wengine kutaka kuamini kuwa huenda kuna ukweli, Diamond amekuwa mkimya licha ya wakati f’lani kuwahi kusema kuwa, hana sababu ya kujibizana na watu wasiojua ukweli kwani yeye anaamini watoto waliozaliwa na Zari ni damu yake.
“Unajua mwanamke akiwa na mimba hupaswi kusema ana mimba yangu maana huna uhakika, lazima uwe na wasiwasi maana ndiyo akili, akishajifungua kama hivi ndiyo unasema ni mtoto wako maana nikimwangalia anafanana kila kitu na Tiffah na ni kopi yangu kabisa,” aliwahi kusema Diamond.
BABA WA DIAMOND ATIA NENO
Katika kutaka kupata maoni ya baba wa Diamond, Mzee Abdul Juma juu ya haya madai kuwa mjukuu wake, Nillan anafanana na Ivan alisema kuwa, katika hali ya kawaida ili kuwazima wale wenye dhana potofu kwamba mtoto si wa Diamond ni lazima vipimo vya DNA vifanyike.
“Mimi kama mzazi namshauri Diamond akapime DNA ili apate uhakika zaidi japokuwa tunaamini hao wajukuu wetu ni watoto wake lakini kwa kuwa maneno yamekuwa mengi kila kukicha ni lazima afanye hivyo, naamini na maneno ya watu kumsimanga yataisha,” alisema Mzee Abdul na kuongeza:
“Katika maisha ya kawaida kwa mwanaume ni aibu kulea watoto ambao unajua kabisa si wako lakini unasema ni wako. Mpaka Diamond anaamini ni watoto wake na sisi ndugu tunaamini hivyo, kwa nini wengine wasikubaliane na ukweli huo.”
DIAMOND ALICHOKIFANYA
Kuhusiana na hili la DNA, watu wamelifananisha na lile na Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda kudaiwa kuwa ana vyeti feki na kuona ni kelele za watu wasiomtakia mema, hivyo kuuchuna. Anachokifanya Diamond ni hichohicho, kukausha akijua ipo siku watu watanyamaza
0 Comments