NAHODHA WA TIMU YA TAIFA, MBWANA SAMATTA
Taifa
Stars - timu ya Tanzania ya mpira wa miguu kwa mwaka 2017 inaingia
uwanjani kucheza na Botswana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
katika mechi ya kirafiki ya kimataifa katika wiki ya kalenda ya FIFA.
Kwa
umuhimu wa mchezo huo na hamasa ambayo uongozi wa Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania umeona hivyo TFF imeatangaza kushusha bei ya kiingilio
kwa watu watakaokaa mzunguko kutoka Sh 5,000 hadi Sh. 3,000.
“Wavutieni
Watanzania wakaishangilie timu yao, wekeni viingilio vya bei ya chini
ambayo Mtanzania itamweka katika mazingira ya kuchangia gharama kidogo
kwa timu. Toeni hiyo Sh 5,000 yenu. Wekeni angalau Sh. 3,000,” ameagiza
Rais wa TFF, Jamal Malinzi.
Pamoja
na punguzo hilo kwa mashabiki wa mpira wa miguu watakaoketi Majukwaa
Maalumu - VIP “A” watalipia Sh 15,000 na wale watakaoketi VIP “B” na “C”
watalipia Sh 10,000.
Kocha
Mkuu wa timu hiyo, Salum Mayanga kwa upande wake aliwathibitishia
Waandishi wa Habari kwamba kikosi chake kiko imara kwa ajili ya mchezo
huo utakaofanyika kuanzia saa 10.00 jioni.
“Tuna morali wa hali ya juu,” alisema Mayanga ambaye aliteuliwa kuinoa timu hiyo mapema mwaka huu.
Kwa
upande wa Peter Buffler – Kocha Mkuu wa Botswana, alisema kwamba
anatarajiwa mchezo wa kesho utakuwa mgumu kwa sababu amegundua kuwa
kikosi cha Taifa Stars kina vijana wengi ikilinganishwa na miaka
iliyopita.
Mbali
ya mchezo huo wa kesho, Taifa Stars inatarajiwa kucheza mchezo mwingine
dhidi ya Burundi Jumanne ijayo, Machi 28, mwaka huu. Mchezo ambao pia
ni wa kirafiki wa kimataifa unatarajiwa kuanza saa 10.00 jioni.
0 Comments