Inaonekana kuna ishu kibao kuhusiana na ajali iliyosababishwa na gari la msanii Jaguar.
Jumanne ya tarehe 21 gari aina ya Range Rover Sport lenye nambari ya usajili KCB 808J ilisababisha ajali liyopoteza maisha ya vijana wawili wa bodaboda. Ajali hii ilitokea katika katika barabara la Makutano kuelekea Sagana mida ya saa tisa za jioni siku hiyo.
Taarifa za awali kutoka kwa mashuhuda zilisema kwamba aliyekuwa kwenye usukani wakati wa ajali alikuwa ni mwanadada fulani anayesemekana kuwa rafiki wa karibu wa msanii huyo wala sio Jaguar aliyekuwa akiendesha gari hilo.
Hata hivyo, cha kushangaza ni kwamba Jaguar aliandikisha taarifa tofauti kabisa katika kituo cha polisi cha Sagana. Kulingana na yeye, aliyekuwa akiendesha wakati ajali hiyo ilipotokea alikuwa ni yeye.
Maneno ambayo yamerudiwa na mkuu wa polisi wa eneo hilo kulingana na ‘statement’ aliyoitoa Jaguar. Hilo linadhihirisha kwamba kuna gemu ya karata inayoendelea kuchezwa. Je, msanii Jaguar anajaribu kufanya ‘cover-up’? Na kama ni kweli, wengi tutajiuliza ni kwanini.
Hii ni ajali ambayo ilipoteza maisha ya vijana ambao familia zao zilikuwa zikiwategemea sana. Hili ni suala lenye uzito sana na halifai kuchukuliwa kuwa nyepesi Kama ni kweli Jaguar anahusika katika kinachoendelea basi atakuwa amefeli kama kiongozi mtarajiwa.
Siku zote sheria lazima ifuatwe na haki itendeke. Kama ilikuwa ni ajali ya kawaida ni kwanini ajaribu kudanganya kuhusu kilichotokea? Naamini vyombo husika vitafuatilia suala hili kiundani zaidi.
0 Comments