Kamishna wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Siro amesema jeshi hilo bado linawashikilia Wasanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya akiwemo Vanessa Mdee ambaye alikamatwa juzi (Jumatano) na Rummy Shaeli kwa tuhuma za matumizi ya dawa za kulevya.
Akiongea na wana habari Ijumaa hii ofisini kwake kamanda amesema jeshi hilo bado linawashikilia watu hao mpaka uchunguzi utakapo kamilika.
“Juzi tulimkamata Vanesa Mdee napia tunamshikilia Rummy Shaeli taarifa zinaonyesha ni watumiaji na wasambazaji lakini upelelezi unaendelea na ukikamilika tutawafikisha mahakamani au tutamuachia. Na sio hao tu wapo wengine ambao tuna majina baadhi tumewakamata inasemekana huwa wanasafirisha dawa hizo kwenda Afrika Kusini,” amesema Siro.
Msanii wa bongo fleva Rummy
Vanessa alikuwa miongoni mwa watuhumiwa wa matumizi ya dawa za kulevya waliotajwa na Mkuu mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda katika orodha yake ya pili na kuwataka kuripoti katika kituo cha kituo kikuu cha polisi. Hata hivyo Vanessa hawakuweza kufika kituoni hapo kwa wakati kwa sababu wakati agizo hilo likitolewa alikuwa nje ya nchi na kumtuma mwanasheria wake kumwakilisha.
0 Comments