Klabu
ya Yanga imeandikiwe barua ya Onyo Kali kutokana na benchi lake la
ufundi kumlalamikia mara kwa mara Mwamuzi wakati wa mechi ya utangulizi
ya U20 kati ya timu hiyo na Simba iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ndiyo lililofikia uamuzi huo ikionekana Yanga imekithiri kwa malalamiko.
Kuhusu mechi za Ligi Daraja la Pili (SDL Play Off)
Mechi
namba 3 (Oljoro 1 vs Transit Camp 1). Klabu ya Oljoro imepigwa faini ya
sh. 200,000 (laki mbili) kutokana na washabiki wa timu hiyo kumrushia
mawe Mwamuzi akiwa uwanjani.
0 Comments