Msanii asiyekaukiwa 'kiki' katika ulingo wa sanaa ya Bongo, Harmorapa
amesimulia kilichomkuta alipokwenda kumuona aliyekuwa Waziri wa habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye kiasi cha kutoka mbio za aina
yake, baada ya kuona bastola.
Harmorapa ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake inayokwenda kwa jina la
'Kiboko ya Mabishoo' aliyomshirikisha Juma Nature, amesema
kilichomfanya aende katika mkutano ule mara baada ya Nape kuondolewa
kwenye nafasi yake ya uwaziri, ni kumpa pole na kumshukuru Nape kwa kuwa
ndiye aliyekuwa mlezi wa tasnia ya sanaa nchini.
Akizungumzia tukio alilolishuhudia la Nape kutishiwa bastola mbele yake,
Harmorapa aliyekuwa akizungumza na eNewz ya EATV, amekiri kuwa ni kweli
hajawahi kuiona kwa ukaribu ule, hivyo alipoona inachomolewa aliogopa
na kujikuta akitoka mbio, huku akikanusha utani ulioenea mitandani kuwa
alikimbia hadi Mtwara.
0 Comments