Usiku wa Alhamisi hii zilichezwa mechi kadhaa katika bara la Amerika
ya Kusini za kufuzu kucheza kombe la dunia mwakani nchini Urusi. Brazil
wakiwa ugenini imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya
Uruguay.
Mabao ya Brazil yalifungwa na Paulinho aliyefunga mabao matatu pamoja na moja la Neymar, na goli lakufutia machozi la Uruguay lilifungwa na Edson Cavan kwa mkwaju wa penati. Katika michezo mingine James Rodrigues wa Real Madrid alifunga bao pekee kwa timu yake ya Colombia na kuisaidia kushinda kwa goli 1-0 dhidi ya Bolivia.
Nao Argentina wakiwa nyumbani walifanikiwa kushinda kwa bao 1-0 dhidi ya Chile. Goli la Argentina lilifungwa na Lionel Messi kwa njia ya penati. Paraguay wakawachapa Ecuador 2-1. Nao Venezuela wakatoshana nguvu na Peru kwa sare ya 2 – 2.

0 Comments