Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina amesema pamoja na kuandamwa na majeruhi mfululizo, kikosi chake kitakuwa sawa.
Lwandamina
amesema washambuliaji wawili wa kati wameendelea kuwa majeruhi kwa
kipindi lakini wengine wameendelea kupambana kwa ajili ya timu jambo
linawapa moyo zaidi.
Majeruhi
ni Donald Ngoma raia wa Zimbabwe na Amissi Tambwe kutoka Burundi ambao
wamekuwa tegemeo la ufungaji na kuongoza mashambulizi ya Yanga.
“Tuna
wachezaji majeruhi na utaona hawajawa vizuri, mazoezi wameanza lakini
si wa kuwategemea. Lakini tunaendelea na maandalizi na wachezaji wengine
wanajituma.
“Imani yetu ni kuendelea kupambana na kuimarisha kila sehemu,” alisema.
Yanga imekuwa ikiendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Polisi Kilwa Road jijini Dar es Salaam.
0 Comments