MABINGWA watetezi Yanga SC inatarajia kukutana na timu ya Azam FC wikiendi bila Nyota wake muhimu wa kikosi cha kwanza.
Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi amefafanua swala hilo kuwa anaandamwa na majeruhi katika kikosi chake.
Yanga itakosa huduma za washambuliaji wake muhimu kama Donald Ngoma na Amisi Tambwe ambao wameendelea kuwa majeruhi hadi sasa wakati mechi ya Yanga vs Azam ikiwa imekaribia.
michael mtanzania ilipiga story na Kocha msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi ambaye amesema:
“Hatuwezi kukata tamaa tutazidi kupambana naamini hao waliopo kwasasa wanaweza kuokoa jahazi siku ya Jumamosi huku safu yetu ya ushambuliaji ikitarajia kuongozwa na Obrey Chirwa.”
“Naomba mashabiki wetu wasikate tamaa katika kipindi hiki wanapaswa watuunge mkono na huku wakiona bado tuna nafasi ya kutetea ubingwa wetu licha ya kuzidiwa alama mbili na watani zetu (Simba),” alisema Mwambusi.
Yanga itaingia uwanjani ikiwa na lengo la kushinda katika mchezo huo ambao unatabiriwa na wengi kuwa mgumu kutikana na rekodi ya hivi karibuni kati ya timu hizo.
Katika muchezo sita iliyopita ya ligi kuu Tanzania bara, timu hizo zimetoka sare mara tano huku Azam ikipata ushindi katika mechi moja.
0 Comments