MICHAEL MTANZANIA

ONESTEPMEDIATZ

Simba inadaiwa Mil 80, nyasi zao bandia zinapigwa mnada leo



KAMPUNI ya udalali ya Majembe Auction Mart imepanga kuzipiga mnada nyasi bandia pamoja na magoli ya timu ya Simba SC kutokana na kukaa bandarini kwa muda mrefu bila kuchukuliwa na wahusika.

Inaelezwa sababu ya kupigwa mnanda kwa nyasi pamoja na magoli yake ni timu ya Simba kushindwa kulipa kodi ya Shilingi milioni 80 wanazodaiwa na TRA.


Mnada huo utakaosimamiwa na Kampuni ya Majembe Auction Mart utafanyika nyuma ya The Waterfront Sunset Restaurant and Beach Bar Barabara ya Yatch Club Masaki Katika ofisi za LW9
Wakati Majembe Auction Mart imetangaza kupiga Mnada wa nyasi bandia na magoli, makamu wa raisi wa Simba Geoffrey Nyange Kabulu ambaye yuko Bukoba na timu amedhibitisha kuwepo kwa mnada huo ila akasema watapambana kabla ya saa nane watakuwa wamepata hizo fedha na kuzuia nyasi hizo kupigwa mnada.

Simba imekuwa ikisuasua tangu mwaka jana nyasi hizo zilipofika Tanzania wakiomba kupata punguzo la kodi kwa sababu ni vitu vya michezo ila hilo hawakuweza kufanikiwa mpaka leo wametangaziwa mnada nyasi hizo zilikuwa zinapelekwa kwenye uwanja wao wa Bunju uliopo Dar.

Post a Comment

0 Comments