Mwamuzi
Jacob Adongo amepewa ONYO KALI kwa kushindwa kutafsiri vizuri sheria
katika mechi namba 186 kati ya Simba na Mbeya City iliyofanyika Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam.
Onyo hilo limetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 38 (5) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.
Kadhalika
katika mchezo huo namba 186 (Simba 2 vs Mbeya City 2). Klabu ya Mbeya
City imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa timu yake kuingia
uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi, hivyo kwenda kinyume na Kanuni
ya 14(14) ya Ligi Kuu.
Adhabu dhidi ya Mbeya City imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(48) ya Ligi Kuu.
Mechi
namba 190 (Kagera Sugar 1 vs Majimaji 0). Klabu ya Majimaji imepigwa
faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa kosa la kutokuwa na Daktari kwenye
Kikao cha Maandalizi ya Mechi (Pre Match Meeting) na hata uwanjani
wakati wa mchezo. Kitendo hicho ni ukiukwaji wa Kanuni ya 14(2b) ya Ligi
Kuu, na adhabu ni uzingativu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Kuu.
Pia
kwa kutumia Kanuni ya 9(8) ya Ligi Kuu imefuta kadi ya njano
aliyooneshwa mshambuliaji Jaffari Salum wa Mtibwa Sugar katika mechi
hiyo namba 175 kati ya African Lyon na Mtibwa Sugar iliyochezwa Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam baada ya kubaini haikuwa sahihi.
0 Comments