Shetta amedai kuwa Shikorobo, wimbo wake aliomshirikisha msanii wa
Nigeria, KCEE, una historia muhimu katika maisha yake ya muziki.
Akizungumza jana kwenye kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz cha EATV ambacho alikuwa host wake, Shetta amesema Shikorobo ni wimbo wake wa kwanza kuimba na alikuwa ana wasiwasi kama watu wengepeipenda.
Amedai mapokezi ya wimbo huo yalikuwa ya maajabu na ndio wimbo ambao umempa pesa nyingi. “Shikorobo ni wimbo ambao nauheshimu sababu umebadilisha asilimia kubwa ya maisha yangu,” amesema.
Hata hivyo rapper na muimbaji ameeleza kuwa video ya Shikorobo ndio iliyomgharimu mkwanja mwingi zaidi kuliko zote alizowahi kufanya.

0 Comments