Dkt Elly Macha (Enzi za uhai wake)
Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Viti
Maalum (CHADEMA) akiwakilisha walemavu Dkt. Elly Macha amefariki dunia
baada ya kuugua kwa muda mrefu.
"Taarifa ni za kweli, mbunge Viti Maalum Dkt. Elly Macha amefariki, lakini sijapata bado taarifa za kina, lakini ninachojua ni kwamba amekuwa akipatiwa matibabu kwa muda mrefu Arusha" Amesema Makene
Miongoni mwa wabunge wa kwanza kutoa taarifa za msiba huyo ni Lazaro Nyalandu ambaye kupitia mtandao wa twitter ameandika "Mbunge mwenzetu, Mhe. Dr. Elly Macha amefariki dunia leo.
Wabunge wote tumeguswa sana na tukio hilo. Upumzike kwa amani dada yetu mpendwa"
Taarifa zaidi kuhusu msiba huu zitaendelea kukujia hivi punde
0 Comments