MICHAEL MTANZANIA

ONESTEPMEDIATZ

Mayanga ametaja sababu za kiufundi za kumuanzishia benchi Mbaraka Tanzania vs Burundi

Inawezakana ulikuwa unajiuliza kwa nini kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Salum Mayanga hakumuanzisha mshambuliaji Mbaraka Yusuf sambamba na Ibrahim Ajib wakati mechi ya kwanza alianzisha washambuliaji wawili Samatta na Ajib.

Mayanga amesema, Mbaraka ilibidi aanzie benchi kutokana na kukosa uzoefu wa mechi za kimataifa
kwa hiyo alihitaji kupata muda wa kuangalia game na kuona wenzake wanafanya nini ili yeye akiingia ajue anatakiwa kufanya nini.

“Kiuzoefu Mbaraka ni mechi yake ya kwanza ya kimataifa, nililazimika kuanza na Ajib ambaye anauzoefu kidogo halafu baada ya hapo nikampa nafasi Mbaraka ili akafanye kile alichokiona kutoka kwa mtangulizi wake.”

“Kwa hiyo kiufundi isingekuwa sahihi kumuanzisha Mbaraka, ilikuwa ni lazima apate kuona nini kinafanyika kwa sababu tulizungumza na nilimuelekeza nini cha kufanya.”

“Yuko vizuri mwepesi wa kuelewa na kushika na  ni mtu wa kujitolea, ameingia ameonesha kwa asilimia nzuri kwamba anaweza akaisaidia timu ya taifa itakayoshiriki mashindano ya CHAN.”

Post a Comment

0 Comments