MICHAEL MTANZANIA

ONESTEPMEDIATZ

Yanga watachomoka kwenye mtego wa Azam?





KIKOSI cha Azam wikiendi hii wataikaribisha Yanga kwenye mchezo wa ligi kuu ambao utapigwa Aprili Mosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar ambapo mechi hiyo inatarajiwa kuwa na ushindani kutokana na mfuatano wa timu hizo kwenye msimamo wa ligi.

Akizingumza na Shaffihdauda.co.tz Kocha Msaidizi wa Azam Iddi Cheche alisema: “Nina amini tunashinda kutoka na kikosi changu kuwa na vijana wenyewe uchu wa kuifikisha mbali Azam.”
“Tunataka kushinda mechi zetu zilizobakia ili kujiweka sawa katika nafasi nzuri ya kushiriki
michuano ya kimataifa,” alisema Cheche.

Azam wapo nafasi ya tatu wakiwa na pointi 44, kama Yanga wakipoteza mchezo huo basi mbio zao za ubingwa zinaweza kufifia rasmi kwa kuwa Simba wapo kileleni zaidi yao kwa pointi mbili na wakishinda dhidi ya Kagera Sugar watakuwa wamewazidi pointi tano ikibaki michezo mitano.

Post a Comment

0 Comments