MICHAEL MTANZANIA

ONESTEPMEDIATZ

Changamoto kubwa anayopambana nayo Farid Musa akiwa Hispania


Winga wa mtanzania Farid Musa anaekipiga kwenye klabu ya Tenerife ya nchini Hispania amesema changamoto kubwa anayopambana nayo tangu ametua Hispania ni lugha inayotumiwa na taifa hilo.
Farid Musa amezungumza na Yahaya Mohamed ‘Mkazuzu’ muda mfupi kabla hajaondoka
Tanzania kurejea Hispania kujiunga na klabu yake baada ya kumaliza majukumu ya kuitumikia Stars kwenye mechi mbili za kirafiki za kimataifa.
“Changamoto kubwa sana niliyokumbana nayo ni lugha yao, sielewi kitu lakini wananifundisha ili tuweze kuelewana na wachezaji wenzangu,” amesema Farid wakati akizungumza na Mkazuzu usiku wa jana kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa Dar es Salaam.
Farid ambaye bado hajaanza kucheza kwenye kikosi cha wakubwa cha Tenerife amesema, baada ya miezi sita kumalizika ataanza kucheza kwenye kikosi cha wakubwa ila kwa sasa anaishia kufanya nao mazoezi tu.
“Naenedelea vizuri mambo yanaenda sawa, nasubiri miezi sita iishe ili niweze kujiunga na timu ya kikosi cha wakubwa. Ninafanya mazoezi na kikosi cha wakubwa lakini sichezi mechi za mashindano.”
Licha ya kucheza katika mechi mbili za kirafiki za Stars ilipocheza na Botswana pamoja na Burundi, Farid amsema hali ya hewa imemsumbua kidogo lakini pia hakufanya mazoezi hata kidogo pamoja na wachezaji wa Stars kwa sababu alichelewa kufika huenda ndio sababu ya kushindwa kuonesha kiwango cha juu zaidi.
“Changamoto niliyokutana nayo ni hali ya hewa, nilikuwa sijafanya mazoezi na timu halafu nimecheza mechi za kimataifa kwa hiyo ilikuwa ngumu kidogo.”

Post a Comment

0 Comments