MICHAEL MTANZANIA

ONESTEPMEDIATZ

Alichokiandika Mwanasheria Alberto Msando kuhusu Msanii Harmorapa


Siku chache baada ya msanii Harmorapa kupata Ubalozi wa kinywaji kinachoitwa cider ‘swala’, Mwanasheria maarufu Alberto Msando ambaye amekuwa akizishughulikia kesi za watu maarufu kama Wema Sepetu na wengineo, ametoa pongezi kwa msanii huyo.

Msando alitoa pongezi hizo kwa Harmorapa kupitia ukurasa wake wa Instagram akimpongeza
kwa hatua aliyopiga na kujitahidi kutengeneza umaarufu ambao wengi wameshindwa. 

Alberto Msando ameyaandika haya kwenye ukurasa wake wa Instagram…
"I really like this guy. @harmorapatz1 sio kwamba ana kipaji kikubwa cha kuimba. Nimesikiliza wimbo wake mmoja. ILA ameweza kutumia fursa. Na kikubwa kuliko vyote AMETHUBUTU. Ameweza kufanya kile ambacho wengi hawawezi.
"Wengi wanasubiri sana kufanya maamuzi. Wengi wanaogopa au wanaona aibu. Nimefurahi leo kuona amepata endorsement ya cider ‘swala’. Its a big step. Hawa ndio vijana ambao tunawataka. Kila nikimuangalia sura yake namkumbuka marehemu Remmy Ongala. Na kuna mtu anamuita baby 😂😂😂😂.;- Msando
"Kisa tu ameweza kuwa na kipato na anaendelea kuwa maarufu. Sitashangaa kusikia wale mastaa wa bongomovie ambao hatujui movie zao wakianza kuvizia malipo ya endorsement!! Na ndio litakuwa anguko lake. Kama wengine. #TheDon#HarmoMbio #HarmoBastola#KiherehereMbeleYaBastolaKinazaaWoga #SuraMkunjo #PuaSasa 😂😂#NusuUsoNusuPua;-Msando

Post a Comment

0 Comments