MICHAEL MTANZANIA

ONESTEPMEDIATZ

Watoto Milioni 152 hawaendi shule wanalazimika kufanya kazi

 
Ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa (UN) imesema Watoto Milioni 152 ulimwenguni wanalazimika kufanya kazi badala ya kwenda shule.

Umoja wa Mataifa (UN),  ulitangaza idadi hiyo ili kujenga uelewa juu ya ajira kwa watoto tarehe 12 June Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Ajira kwa Watoto.

Kwa mujibu wa ripoti ya November 2017 ya Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF), karibu moja kati ya watoto wanne katika nchi zilizoendelea zaidi wanalazimika kufanya kazi zinazoathiri afya zao na maendeleo.

Shirika la Kazi la Kimataifa (ILO) linaelezea kazi ya watoto kama jambo linalozuia utoto wao, linaharibu uwezo wao, maendeleo yao ya kimwili na ya akili.”
kulingana na ripoti ya ILO ya 2017, kuna wafanyakazi watoto milioni 152 kati ya umri wa 5-17.
Ingawa kiwango cha ajira kwa watoto kinapungua kila mwaka, ni muhimu kutambua kuwa kiwango hicho hakipungui kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Kati ya watoto milioni 152, milioni 73 wanafanya kazi za hatari

Post a Comment

0 Comments