MICHAEL MTANZANIA

ONESTEPMEDIATZ

Askari hufukuzwa kazi kutokana na Utoro

Kamanda wa polisi kanda maalum ya dar es salaam, SACP Lazaro Mambosasa amesema kuwa kazi ya jeshi ni kusimamia sheria, kuna kamati mbalimbali ambazo ni kusimamia maadili kwa wanaopokea rushwa,  ambapo kwa askari ambae kwao anabainika kupokea rushwa hatua huchukuliwa kwa kufikishwa kwenye kamati na hatua za kijeshi kuchukuliwa pamoja na kufukuzwa kazi iwapo hatabadilika. 
Amesema kuwa anawashukuru wananchi kwa kuwa wao ni chanzo kikubwa cha kutoa taarifa juu ya uhalifu,  vilevile amesema kuwa askari wengi wamefukuzwa kazi kutokana na utoro jeshini ambao huvumiliwa kwa siku tano. Ikizidi hapo hufukuzwa kazi na kusisikiza kuwa askari yoyote anaposafir kwenda popote hupewa hati ya kusafiria ambayo itaonyesha anapotokea na atakapofikia. 

Mambosasa amesema kuhusiana na matukio ya utekaji kwasasa dar es salaam iko shwari pamoja na fukwe za bahari,  vilevile amesema wananchi kukutwa wamekufa na kufungwa na mifuko ya sandarusi amesema kuwa hiyo ilishatolewa ufafanunuzi na IGP na hivyo anaamini kuwa hayo matukio hayatokei kwenye nchi yetu

Post a Comment

0 Comments