MICHAEL MTANZANIA

ONESTEPMEDIATZ

KELVIN DU RANT MTOTO ANAYETISHA NBA

WABISHI Golden State wamefanya mambo makubwa tena baada ya kufanikiwa kutwaa ubingwa wa NBA, baada ya kuwachapa Cleveland Cavaliers, kwenye michezo 4-0 ya fainali.



Huu ni ubingwa wa pili mfululizo kwa wanaume hao, lakini ukiwa ubingwa wao wa tatu kati ya minne ya hivi karibuni, hakika wanastahili pongezi.

Lakini pamoja na timu hiyo kutwaa ubingwa huo wa NBA, mwanaume Kevin Durant naye alifanya maajabu tena baada ya kufanikiwa kutwaa tuzo ya MVP.

Tuzo hii ni sawa na kuiita Mchezaji Bora wa Fainali za NBA, au Mchezaji Bora wa NBA kwa mwaka husika na Durant amewafunika wote huku akiiongoza timu yake kutwaa ubingwa huo muhimu mwaka huu.

Durant mwenye urefu wa futi sita na inchi 11, alifanya kazi kubwa kwenye fainali za mwaka huu kama alivyofanya mwaka jana.

“Ni suala la safari ya msimu mzima, kuamka kila siku kwenda kufanya kazi ukiwa na timu bora kama hii ni jambo zuri na linalovutia.

“Mazingira ya timu hii yanakufanya unaonyesha kiwango cha hali ya juu, kila mmoja ana uwezo wa hali ya juu kwenye timu hii ndiyo maana tunafanikiwa,” alisema staa huyo.

Post a Comment

0 Comments