MICHAEL MTANZANIA

ONESTEPMEDIATZ

Antoine Griezmann awaziba mdomo wanao mfuatilia ‘Nimeshafanya maamuzi ya wapi pakwenda’


Baada ya kuwepo kwa maneno mengi juu ya hatma ya straika wa klabu ya Atletico Madrid, Antoine Griezmann hatimaye amevunja ukimya na kusema kuwa tayari ameshafanya maamuzi juu ya timu gani atakwenda kuichezea msimu ujao.



Griezmann amekuwa akihusishwa na kutakiwa na klabu kubwa barani Ulaya zikiwemo Manchester United na Barcelona baada ya kuonyesha kiwango kikubwa msimu uliyopita kwa kuifungia timu ya Atletico mabao 29 kwenye michezo yake 49 aliyocheza.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, ameyasema hayo kwenye mkutano wake na waandishi wa habari huko nchini Urusi wakati akiwa na kwenye majuku ya michuano ya kombe la Dunia na timu yake ya taifa ya Ufaransa huku akishindwa kusema anaelekea klabu gani ama atasalia Altletico.

Post a Comment

0 Comments