Kiungo Mshambuliaji wa Timu ya Singida United,Deus Kaseke hatutakuwa naye msimu ujao baada ya kupata dili nchini Afrika Kusini kucheza Mpira wa kulipwa na kuzima tetezi ambazo zinadai kuwa taungana na kocha wake wa zamani Hans Van Der Pluijm aliyejiunga na Azam FC
Festo Sanga amekanusha taarifa za muda mrefu ambazo zimekuwa zikimhusisha Kaseke kujiunga na Azam kutokana na uhusiano wake mzuri na Hans van Pluijm ambaye ametangazwa kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo.
“Deus Kaseke amepata ofa kutoka South Afrika, kuna timu imepanda ligi kuu ya huko inamuhitaji Kaseke. Sina taarifa kwamba anakwenda kuungana na kocha Hans”-Festo Sanga.
Kaseke alijiunga na Yanga wakati Pluijm akiwa kocha mkuu wa ‘timu ya wananchi’ wawili hao wakaungana tena Singida United inawezekana ndiyo sababu ya kuhusishwa tena kutaka kufanya kazi pamoja Azam FC.
0 Comments