MICHAEL MTANZANIA

ONESTEPMEDIATZ

YANGA BADO NAFASI IPO KOMBE LA SHIRIKISHO

Matokeo ya suluhu kwenye mchezo wa Yanga dhidi ya Rayon Sports katika Kundi B la michuano ya kombe la shirikisho Afrika bado Yanga ina nafasi ya kufanya vizuri kwenye kundi hilo kutokana na matokeo ya timu nyingine za kundi hilo.

Yanga ina pointi moja baada ya kucheza mechi mbili ikiwa nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa Kundi B ambalo kinara wake ni USM Alger yenye pointi nne huku Gor Mahia na Rayon Sports zikiwa na pointi mbili baada ya Gor Mahia kutoka suluhu na USM Alger.
Yanga bado hawajaondoka moja kwa moja katika harakati za kutafuta nafasi mbili za juu ili kusonga mbele katika hatua inayofuata.
Michezo ya kimataifa ina aina maandalizi ya aina yake, baada ya draw kuchezeshwa na timu Yanga kujikuta ipo Kundi B pamoja na timu za USM Alger, Gor Mahia na Rayon Sports ‘on pepers’ watu wengi waliamini hili ni kundi jepesi sana.
Kiuhalisia ni kundi ambalo lipo fair sana kwa kila timu kuweza kufuzu hatua ya mtoano kwa kutegemea na maandalizi ya timu husika. Kwa hiki ambacho kimetokea leo haikuwa miujiza, Rayon Sports walikuwa wamejipanga kupata matokeo ugenini na wamefanikiwa kupata sare.
Sare ya USM Alger na Gor Mahia inaweza kuwaweka Yanga mahali pazuri endapo watapata matokeo kwenye mchezo ujao, lakini bila maandilizi wala mipango ya kuingia kwenye mechi husika kwa maana ya mwalimu pamoja na benchi la ufundi lakini pia aina ya wachezaji wanaowatumia katika mechi inaweza kuwa changamoto kwa Yanga na kuendelea kukosa matokeo kwenye michezo yao.
Benchi la ufundi watakuwa wamepata kitu baada ya sare ya leo kuelekea mchezo ujao.

Post a Comment

0 Comments