Timu ya soka ya Tanzania ya watoto wa kike wanaoishi katika mazingira magumu, imefungwa kwa mbinde goli 1-0 na timu ya Brazil katika fainali ya Kombe la Dunia( Street Children World Cup)
-
Kwa matokeo haya timu hiyo imeshika nafasi ya pili katika michuano hiyo iliyoandaliwa na Shirika la Street Child United na kufanyika nchini Urusi
-
Timu hiyo ya Tanzania mpaka inaingia hatua ya fainali ilikuwa haijapoteza mchezo hata mmoja na hivyo mchezo wa fainali waliofungwa ndio mchezo pekee waliopoteza
-
Itakumbukwa kuwa mwaka 2014 nchini Brazil, timu ya wavulana walio kwenye mazingira magumu ilichukua ubingwa kwa kuifunga Burundi.
0 Comments