Aliyewahi kuwa Kocha Msaidizi ndani ya Simba, Jamhuri Kihwelo 'Julio' amepinga suala la Mwanachama atakayetakiwa kugombea nafasi ya urais ndani ya klabu hiyo mara baada ya mfumo wa kisasa kuanza ni lazima awe na Shahada.
Kufuatia mchakato wa mabadiliko ya katiba kukamilika baada ya wanachama kuridhia Jumapili ya wiki jana, muundo mpya wa kisasa utakaoandaliwa utampasa Mwanachama atakayehitaji kugombea nafasi hiyo ya juu ya Urasi kuwa lazima awe na Shahada.
Kutokana na maamuzi hayo, Julio amesema Wanasimba wengi hawajasoa hivyo itakuwa ni mtihani mkubwa kupata watu wa aina hivyo ni vema kiwango cha elimu kikashuka kidogo.
Julio ambaye ni Kocha wa Dodoma FC kwa sasa ameeleza hayo kutokana na asilimia kubwa ya Wanachama wa Simba hawana elimu ya kiwango cha juu hivyo watakuwa kama wamebana fursa kwa kuwa hata yeye angependa kuipata nafasi hiyo.
Julio ameeleza kuwa naye ni mmoja wa watu ambao wanahitaji kupata nafasi ya kugombea wadhifa huo lakini kutokana na kiwango cha elimu kilichowekwa inakuwa ngumu kwake.
Mbali na hayo, Julio amempomgeza Mohammed Dewji kwa kuamua kuwekeza Simba akiamini ni mwanzo wa mafanikio wa klabu hiyo ambayo itakuwa katika taswira tofauti kabisa kuanzia msimu ujao.
0 Comments