MICHAEL MTANZANIA

ONESTEPMEDIATZ

INAELEZWA FEDHA ZA MAJARIDA NA KALENDA YANGA ZAISHIA MIFUKONI HUKU KLABU IKIYUMBA KIUCHUMI

Wakati hali ya kiuchumi Yanga ikionekana kuwa mbaya kwa siku za hivi karibuni, inaelezwa kuwa fedha zilizotokana na mauzo ya jarida pamoja na kalenda za klabu hiyo zimeishia mifukoni kwa matumizi binafsi.


Taarifa zilizopo zinasema kuwa asilimia kubwa ya mapato yaliyopatikana kwa mauzo ya bidhaa hizo zimeenda mifukoni mwa baadhi ya viongozi wa Yanga huku klabu ikihaha na hali mbaya kiuchumi.

Kupitia kipindi cha michezo cha Radio EFM, Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, ameshindwa kuliweka wazi sakata hilo la kupotea kwa fedha akidai kuwa yuko barabarani akiomba atafutwe baadaye.

Ikumbukwe miezi kadhaa iliyopita uongozi wa klabu hiyo ulianzisha jarida maalum na kalenda zenye jina la timu zililokuwa zinatoa taarifa maalum kuhusiana na wachezaji wake.

Lakini jarida hilo lilishindwa kudumu baada ya kuwa sokoni kwa muda mfupi na baadaye uongozi ulikuja na taarifa kwa kueleza kuwa mauzo hayakuwa mazuri hivyo ikabidi lisitishwe ili kujipanga upya.

Post a Comment

0 Comments