MICHAEL MTANZANIA

ONESTEPMEDIATZ

BAADA YA WANACHAMA KURIDHIA MABADILIKO YA KATIBA, UONGOZI SIMBA WATAJA KIPI KITAKACHOFUATA

Uongozi wa klabu ya Simba umeweka wazi kuhusiana na kile kitakachofuata ili kukamilisha rasmi mchakato wa mabadiliko ya uendeshwaji wa klabu hiyo kwa mfumo wa hisa.

Baada ya wanachama kuridhia kufanya mabadiliko ya katiba jana kwa kukubali mwekezaji inabidi achukua asilimia 49 huku wanachama wakichukua 51, uongozi umesema kitakachofuata hivi sasa na kuifikisha kwa msajili.
Simba itaipeleka katiba hiyo kwa msajili wa serikali ili kuisajili katiba hiyo, kisha hatua itakayofuatia ni kuanza kutengeneza muundo utakaoenda kwa jina la Simba Sports Club Company Limited ambao utahusika na shughuli zote za klabu hiyo.
Baada ya hatua hizo mbili kukamilika, tayari klabu itakuwa imeshakamilisha mchakato mzima kwa asilimia 100 na tayari mfumo huo utakuwa umeshaanza kazi.

Post a Comment

0 Comments