Zulu anaungana na Donald Ngoma pamoja na Amis Tambwe ambao ni
wachezaji muhimu wa kikosi cha kwanza wanaosumbuliwa na majeraha.
Kocha msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi amesema kucheza mashindano mengi mfululizo bila kupumzika ndio sababu kubwa ya wachezaji wao kupata majeraha.
“Tatizo la majeruhi linalotukabili sasa hivi linatokana na wachezaji kukosa muda wa kupumzika baada ya mashindano. Msimu uliopita tulikuwa na mashindano ya ligi kuu, FA Cup, tukaingia ligi ya mabingwa baada ya hapo tukahamia kwenye kombe la shirikisho halafu hatukupata muda wa kupumzika tungaunganisha na ligi kuu msimu huu. Kwa hiyo kama hujajiandaa vizuri lazima utakumbwa na wimbi la majeruhi.”
“Majeruhi wanaongezeka, hiki kitu kina tugharimu sana, sisi kama waalimu tunasikitika kwa sababu tunazidi kupunguza wachezaji ukizingatia tunaenda kwenye mashindano muhimu sana. Kwa sasa lengo letu kuu ni kwenye mashindano ya Afrika kwa sababu huku ubingwa wa ligi tumeshashinda mara nyingi.”
Juma Abdul amerejea uwanjani baada ya kupambana na majeraha kwa muda mrefu na alikuwa sehemu ya wachezaji waliocheza kwa dakika 90 dhidi ya Azam na kuisaidia timu yake kupata pointi tatu.
0 Comments