Tukio la Himid kumuumiza Zulu lilitokea dakika ya
30 kipindi cha kwanza wakati Himid akijaribu kumzuia Zulu asipige shuti golini kwa Azam. Zulu alipata jeraha kwenye mguu wake wa kushoto na kushindwa kuendelea na mchezo hali iliyopelekea kutolewa nje ya uwanja kwa msaa wa machela na kukimbizwa haraka kwenye zahanati iliyopo uwanjani kwa ajili ya matibabu zaidi.
“Nampa pole mchezaji wa Yanga Justine Zulu kwa kuumia, haikuwa nia yangu kumuumiza ni bahati mbaya, pia nilienda kumpa pole halftime,” ni ujumbe aliouandika Himid Mao kwenye account yake ya twiter.
Kwa mujibu wa account ya Instagram ya Yanga (yangasc), wamepost picha inayoonesha jeraha alilopata Zulu na kusema kwamba, ameshonwa nyuzi tisa (9).
Himid pia kupitia twiter amewapongeza wachezaji wenzake kwa mchezo mzuri licha ya kupoteza mechi yao dhidi ya Yanga.
“Matokeo hayakuwa mazuri kwa upande wetu, nawapongeza wachezaji wenzangu kwa kucheza vizuri japo hatujashinda mechi,” Himid Mao.
0 Comments