Michezo ya leo itakuwa kati ya
Mabingwa watetezi wa VPL, Young Africans na Azam – mechi itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati mchezo mwingine utakuwa ni kati ya Mbeya City na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Mechi zote zitaanza saa 10:00 jioni.
Mechi za ligi hiyo ambazo huoneshwa mubashara na Kituo cha Televisheni cha Azam ambacho ni mdhamini mwenza wa VPL, itaendelea kesho Jumapili April 2, 2017 ambako Kagera Sugar inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Simba kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera. Mchezo huo utakuwa saa 10:00 jioni.
Mchezo mwingine utazikutanisha timu za African Lyon ya Dar es Salaam dhidi Stand United ya Shinyanga utakaofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Mchezo huu, utaanza saa 8:00 mchana kwa kuwa kanuni zinaridhia.
Mtibwa Sugar ya Morogoro watakuwa wageni wa Tanzania Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Sokoine jijini humo wakati Mwadui FC, kwa upende wake watawaalika JKT Ruvu ya Pwani kwenye Uwanja wa Mwadui huko Shinyanga huku Majimaji wakiwa ni wenyeji wa Toto Africans kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.
0 Comments