MICHAEL MTANZANIA

ONESTEPMEDIATZ

Mavugo ahaidi goli Kagera Sugar

MSHAMBULIAJI WA SIMBA, LAUDIT MAVUGO.

MSHAMBULIAJI wa Simba, Laudit Mavugo, amesema ana uhakika wa kufunga kwenye mchezo wa kesho wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar.

Mchezo huo ni kati ya michezo mitatu ambayo Simba itacheza kanda ya ziwa katika kipindi cha wiki mbili.

baada ya mchezo wa kesho, Simba itaelekea Mwanza kuumana na timu mbili za jiji hilo, Mbao FC na Toto African.

Akiuzungumzia mchezo wa kesho, Mavugo, alisema kuwa anafahamu ugumu wa mechi hiyo lakini amejipanga kuhakikisha anafunga na kupigania ushindi kwa timu yake.

"Tumekuja huku (Kagera) kwa lengo la kushinda mchezo wetu, kama mshambuliaji kazi yangu ni kufunga na kusaidia timu kufanya vizuri..., nitapambana kuhakikisha nafanya hivyo," alisema Mavugo alipoongea na gazeti hili.

Alisema kuwa pamoja na kuwa mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na wenyeji wao nao kuhitaji ushindi, bado anakipa nafasi kubwa kikosi chake kuibuka na ushindi.

Aidha, alisema ushindi kwenye mchezo huo wa kesho utawapa hamasa kubwa na kuwapandisha molali kuelekea kwenye michezo yao ya Mwanza.

"Tukipata ushindi kwenye mchezo wa huku Kagera, ni wazi tutaenda Mwanza molali yetu ikiwa juu," alisema Mavugo.

Simba itacheza na Mbao FC Aprili 10 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba kabla ya kuwavaa Toto African siku tatu baadae.

Post a Comment

0 Comments