MICHAEL MTANZANIA

ONESTEPMEDIATZ

Viwango vipya vya soka vilivyo tolewa na FIFA

Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kila mwezi kwa sasa limekuwa likitoa viwango vipya vya ubora duniani ambavyo vinaonyesha baadhi ya mataifa kupanda katika nafasi .

Kwa upande wa orodha ya jumla, Argentina bado wameendelea kuwa vinara wakifuatiwa na Brazil katika nafasi ya pili huku mabingwa wa dunia Ujerumani wakiwa nafasi ya tatu.

Kwa upande wa Afrika ; Uganda bado wanaendelea kuongoza kwa Afrika Mashiriki wakiwa nafasi ya 16 kwa Afrika na 74 duniani wakifuatiwa na Kenya waliopo nafasi ya 21 Afrika na 88 duniani wakati Rwanda wako nafasi ya 24 Afrika na 93 duniani na Burundi nafasi ya 41 Afrika na 139 duniani.

Misri wao wameendelea kuwa vinara kwa kukwea kwa nafasi mbili zaidi hadi nafasi ya 20, wakifuatiwa na Senegal walioko nafasi ya 28 huku mabingwa wa michuano ya Mataifa ya Afrika Cameroon nao wakikwea kwa nafasi moja mpaka nafasi ya 32 duniani.

Mabingwa wa Amerika Kusini Chile wapo nafasi ya nne na Ubelgiji ndio wanakamilisha tano bora kwenye orodha hizo.

Tanzania imepanda kwa nafasi moja katika viwango kwa nafasi ya 158

Post a Comment

0 Comments