MICHAEL MTANZANIA

ONESTEPMEDIATZ

ZANACO WAMTAZAMA MSUVA KWA JICHO LA TATU MECHI YA MARUDIANO

Simon Msuva ndiye mchezaji atakayewekewa ulinzi mkali zaidi wakati Yanga itakaporudiana na Zanaco mjini Lusaka, Zambia.


Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga wametoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Zanaco ambao ni mabingwa wa Zambia katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, jana.

Nahodha wa Zanaco, Zeyo Tembo amesema, Msuva ndiye mchezaji hatari zaidi katika kikosi cha Yanga na watamfanyia kazi.

“Yule namba ishirini na saba, alikuwa kila sehemu uwanjani. Amefunga lakini alikuwa akisaidia mashambulizi mengi kuja kwetu.

“Tokea awali tulijua Yanga ni hatari kutokea kulia. Hilo limethibitika tena. Lazima tulifanyie kazi zaidi ikiwa ni pamoja na Msuva,” alisema Tembo.
Ilikuwa mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, atakayeteleza, basi anaangukia kwenye Kombe la Shirikisho.

Yanga ina kazi ngumu katika mchezo ujao mjini Lusaka na lazima ijiandae kwelikweli.

Post a Comment

0 Comments